Taasisi ya RUDI inatambua umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi wenye malengo ya kuendeleza biashara, kuongeza tija na thamani za bidhaa/ mazao uuganishaji masoko na kujenga uwezo kwa vikundi husika na kuendeleza uchumi mjini na vijijini.
Ili kutimiza malengo yake RUDI itafanya kazi na wafuatao:
- Serikali ya vijiji, kata na halmashauri za wilaya/ miji
- vikundi vya wajasiriamali/ wafanyabiashara, wakulima, wauza pembejeo, chemba za wenye viwanda na kilimo (TCCIA) na mashirika ya wakulima.
- Vyombo vya fedha ikiwa ni pamoja na vyombo vya kuweka na kukopa, taasisi za fedha n.k
- Wahisani
- Mashirika yasiyo ya serikali ndani na nje ya Tanzania
- Sekta binafsi, watoa huduma, wanunuzi wa mazao n.k
- Mabaraza ya biashara ngazi ya wilaya na mkoa.
|