RUDI:
Taasisi ya maendeleo vijijini na mjini (RUDI) ni taasisi isiyo ya serikali iliyosajiliwa na inafanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania.
MALENGO YA TAASISI YA RUDI :
Shughuli za taasisi ya Rudi zinalenga kujenga/ kuanzisha/ kuimarisha vikundi/ vyama vya wakulima na vya wafanyabiashara/ wajasiliamali ili viweze kufanya yafuatayo
- Kuanzisha/kuimarisha vikundi vya wajasiliamali, wakulima, vyama vya kuweka na kukopa na mashirikisho (APEX) ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa endelvu.
- Kuibua sera ambazo zinazozorotesha ufanisi wa shughuli zao na kuzijadili kwenye vikao mbalimbali kuanzia halmashauri za wilaya/ miji hadi serikali kuu.
- Kuunganisha vikundi vya wakulima na masoko mazuri ndani na nje ya nchi.
- kuwezesha vikundi vya wafanyabiashara/ wajasiliamali na wakulima ili vipate taarifa ya masoko kupitia tovutia tovuti, simu nk.
- kutoa elimu ya kilimo cha biashara kwa vikundi/ vyama vya wakulima ili waweze kujua faida na hasara inayopatikana kwenye kilimo
- kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vikundi vya wajasiriamali, wakulima ili viweze kufanya biashara yenye faida.
- Kutoa elimu ya kilimo bora na ya usindikaji ili wakulima waongeze ubora,tija na thamani ya mazao.
- Kuunganisha vikundi vinavyojipanga na serikali kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi wilaya ili vifahamu mipango/ sera za serikali kuhusu kilimo n.k (ASDP, Padep, Mkuabita, Mkukuta n.k)
- Kuandaa mikutano ya wadau wa maendeleo kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya
- Kushirikiana na TCCIA na halmashauri za wilaya kuanzisha mabaraza ya biashara
- Kushirikiana na vikundi na mashirikiano ya wakulima kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani (WRS).
|